Simba Sports Club
Uncategorized

Tumegawana pointi na Yanga

30 Apr 2022 By simbasc 675 views

Mechi yetu ya Ligi Kuu ya NBC ya Derby dhidi ya Yanga iliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa imemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida timu zikicheza soka la mbinu na kusomana huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Makipa wa timu zote hawakupata misukosuko kipindi cha kwanza kutokana na idadi chache ya mashambulizi yaliyotengenezwa.

Advertisement

Kipindi cha pili tuliongeza kasi kidogo na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini hata hivyo hatukuzitumia ipasavyo.

Kocha Pablo aliwatoa Clatous Chama, Sadio Kanoute, Bernard Morrison na Pape Sakho na kuwaingiza Rally Bwalya, Mzamiru Yassin, Kibu Denis na John Bocco.

Back to homepage
Share this story