Simba Sports Club
Newe

Timu yaendelea kujifua Mo Arena

13 Oct 2022

Timu ilianza mazoezi juzi Jumanne na jana iliingia kambini rasmi kujiandaa na mchezo huo muhimu ambao utatupa tiketi ya kufuzu hatua ya makundi.

Wachezaji wawili Shomari Kapombe na Jimmyson Mwinuke ambao ni majeruhi ndiyo pekee hawakufanya mazoezi lakini wengine wote wameshiriki na wapo katika hali nzuri.

Advertisement

Winga Peter Banda ambaye alipata maumivu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kipanga FC ameshiriki asilimia 100 mazoezi hayo huku akiwa fiti tayari kwa De Agosto.

Back to homepage
Share this story