Simba Sports Club
First Team

Simba yapaa kuelekea Morocco kwa 'Pre Season'

10 Aug 2021

Kikosi chetu kimeondoka nchini mchana huu kuelekea Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22 (Pre Season) kikiwa na wachezaji 24.

Kambi hiyo itakuwa ya wiki mbili na timu itarejea nchini kwa ajili ya kumalizia maandalizi kabla ya kuanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi kuu mwishoni mwa Septemba.

Advertisement

Tumeamua kwenda kuweka kambi nchini Morocco kwa kuwa tunafahamu tutapata utulivu na kuwaweka wachezaji wetu vizuri kabla ya kuanza msimu.

Baada ya timu kurejea, kutakuwa na siku chache kabla ya Tamasha kubwa la Simba Day (lini?) ambapo tutatambulisha wachezaji..

Back to homepage
Share this story