Simba Sports Club
Queens

Simba Queens yakabidhiwa kombe lake

13 Jul 2021

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens, imekabidhiwa taji lake la Ubingwa wa Ligi (Serengeti Lite Women Primier League) baada ya kumalizika mchezo maalumu dhidi ya Twiga Stars leo.

Baada ya mchezo huo maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru fursa ya kukabidhiwa ubingwa umemalizika kwa kupoteza mabao 2-1.

Advertisement

Bao letu pekee kwenye mchezo huo limefungwa na kinara Oppa Clement dakika ya 81.

Simba Queens imemaliza Ligi ya Wanawake ikiwa na pointi 51 ikicheza mechi 19 na kushinda 16 huku ikitoka sare tatu.

Back to homepage
Share this story