Simba Sports Club
Caf Champions League

Simba kukutana na Wabotswana Ligi ya Mabingwa Afrika

18 Sep 2021

Timu yetu itakutana na Jwaneng Galaxy kutoka Botswana katika hatua ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu wa 2021/22.

Simba ni miongoni mwa timu 10 ambazo hazijaanza hatua ya awali kutokana na mafanikio tuliyopata msimu uliopita ya kufika robo fainali ya michuano hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Jwaneng utakuwa kati ya Oktoba 15 na 16 nchini Botswana kabla ya kurudiana hapa nchini.

Advertisement

Jwaneng imetinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Diplomates FC ambapo walishinda mchezo wa kwanza mabao mawili huku wakipoteza mechi ya marudiano iliyopigwa leo.

Endapo tutaibuka na ushindi wa jumla ya mechi zote mbili dhidi ya Jwaneng tutakuwa tumeingia moja kwa moja hatua ya makundi.

Back to homepage
Share this story