Simba Sports Club
Ligi Kuu

Simba kuanzia Mara Ligi Kuu 2021/22

10 Sep 2021

Ratiba ya Ligi Kuu Msimu wa 2021/22 imetoka na mchezo wetu wa kwanza utakuwa ugenini katika Uwanja wa Karume mkoani Mara dhidi ya Biashara United, Septemba 28.

Kampeni yetu ya kutetea taji la ligi kuu itaanza mkoani Mara kabla ya kuelekea jijini Dodoma kuikabili Dodoma Mji kwenye mechi ya pili itakayopigwa Oktoba Mosi.

Mchezo wetu wa kwanza wa nyumbani msimu huu utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Oktoba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Advertisement

Baada ya mchezo huo tutabaki tena nyumbani kuikabili Coastal Union kwenye mchezo wetu wa nne wa ligi ambao utakuwa Oktoba 31.

Mechi yetu ya tano itakuwa dhidi ya Namungo FC ambayo tutakuwa nyumbani pia mtanange utakaopigwa Novemba 3, Benjamin Mkapa.

Mchezo wetu wa Derby dhidi ya watani Yanga umepangwa kufanyika Desemba 11 saa 11 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Back to homepage
Share this story