Kikosi chetu leo kinaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga.
Mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi Jula 3, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, inasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka ndani na nje ya nchi ambapo inatarajiwa kuwa na msisimko hasa baada ya ile ya awali kuahirishwa.
Kikosi chetu kilianza mazoezi jana jioni kwenye viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kuelekea mchezo huo na leo kimeingia rasmi kambini.
Advertisement
Maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na kila kitu kimekaa mahali pake.
Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu lengo letu ni kuhakikisha tunatawazwa rasmi mabingwa wa ligi kwa kuifunga Yanga Jumamosi.