Simba Sports Club
Caf Women's

Oppa kuongoza mashambulizi dhidi ya Lady Doves

31 Aug 2021

Mshambuliaji kinara wa Simba Queens, Oppah Clement atakiongoza kikosi chetu katika mchezo wa pili wa Michuano ya Caf Women's Champions League Cecafa Qualifier 2021 dhidi ya Lady Doves kutoka Uganda leo katika Uwanja wa Moi Kasarani.

Opa amejiunga na wenzake juzi na alikosa mchezo wa kwanza dhidi ya PVP FC tulioibuka na ushindi wa mabao 4-1 kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo yamemalizika na amerejea kikosini.

Opa ndiye mfungaji bora wa kikosi chetu katika msimu uliopita wa ligi ya Wanawake 'Serengeti Lite Women's Champions League' hivyo tunaamini atafanya vizuri kwenye mchezo wa leo.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

1. Zubeda Mongi

2. Dotto Evarist

3. Violeth Nicholaus

4. Julieta Singano

5. Fatma Issa

6.Joelle Bukuru

7.Danai Bhobho

8.Zena Khamis

9. Mawete Musolo

Advertisement

10. Oppa Clement

11. Ruth Kipoi

Wachezaji wa Akiba

Janeth Shija

Gelwa Yona

Maimuna Hamis

Silvia Thomas

Violeth Thadeo

Jackline Albert

Koku Kipanga

Aisha Juma

Shelda Boniface

Asha Kadosho

Back to homepage
Share this story