Simba Sports Club
Uncategorized

Opa akabidhiwa tuzo yake ya Januari

17 Feb 2022 By simbasc 919 views

Mshambuliaji kinara wa Simba Queens, Opa Clement jana alikabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi Januari wa Serengeti Lite Women's Premier League.

Opa alikabidhiwa tuzo hiyo na wadhamini Rani Sanitary Pad sambamba na kitita cha Sh 500,000 baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Fountain Gate.

Advertisement

Katika mwezi Januari, Opa amefunga mabao 10 katika michezo sita tuliyocheza huku akifanikiwa kufunga mabao matatu (hat trick) moja.

Opa anakuwa mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo hiyo ambayo ni mpya na imeanza kutolewa Januari mwaka huu.

Back to homepage
Share this story