Simba Sports Club
Mugalu

Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Khouribga

26 Aug 2021

Mshambuliaji Chris Mugalu amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Olimpique Club Khouribga hapa Morocco utakaoanza saa 12 kwa saa za nyumbani.

Mugalu amekuwa na mchango mkubwa kwa timu anapoanzishwa mshambuliaji pekee kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaa na mpira na kuwasumbua mabeki.

Katika mchezo wa leo, langoni atasimama Ally Salim kutokana na mlinda mlango Aishi Manula kurejea nchini Tanzania kutumikia timu ya Taifa huku Beno Kakolanya akiwa kwenye msiba wa mama yake.

Advertisement

Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison leo ameanza kama mlinzi wa kulia, Gadiel Michael akiwa kushoto katikati akisimama Pascal Wawa na Henock Inonga Baka.

Sadio Kanoute atacheza kama kiungo wa ulinzi akisaidiana na Rally Bwalya huku Hassan Dilunga na Duncan Nyoni wakitokea pembeni.

Kikosi kamili kilivyopangwa, Ally Salim, Bernard Morrison, Gadiel Michael, Pascal Wawa, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Hassan Dilunga, Pape Ousmane Sakho, Chris Mugalu na Duncan Nyoni.

Back to homepage
Share this story