Simba Sports Club
RIPHansPoppe

Msiba wa Hans Poppe upo Ununio

11 Sep 2021

Msiba wa aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu yetu, Zakaria Hans Poppe aliyefariki usiku wa kuamkia leo upo nyumbani kwake Ununio jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuwa Mjumbe wa Bodi, Hans Poppe alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu na amefanikisha kupatikana kwa nyota wengi wazuri ndani ya Simba.

Advertisement

Kutokana na janga la Uviko 19 hakutakuwa na mkusanyiko wa msiba zaidi ya ndugu na jamaa wa karibu nyumbani hapo.

Kuhusu ratiba mazishi yatakapofanyika itatolewa na ndugu wa marehemu ambapo katika shughuli ya kuaga watu wote wataruhusiwa.

Back to homepage
Share this story