Simba Sports Club
Uncategorized

Mgunda: Tunaelekeza nguvu zetu Angola

3 Oct 2022 By simbasc 343 views
Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji tuliopata jana sasa tunaelekeza nguvu katika mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto ya Angola ugenini. Kauli hiyo imetolewa na kocha mkuu, Juma Mgunda ambapo amesema maandalizi dhidi ya De Agosto yameanza mara moja kabla ya kikosi kupaa kuelekea Angola. Mgunda ameongeza kuwa mapungufu yaliyoonekana kwenye mchezo wa jana yatafanyiwa kazi mazoezini kabla ya kukutana na De Agosto mwishoni mwa juma lijalo. "Tunamshukuru Mungu tumepata ushindi mnono kabla ya mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa, utatuongezea morali katika mechi yetu ya ugenini nchini Angola. "Maandalizi ya mchezo huo tayari yameanza na kitu kizuri hatutakuwa na mchezo wa ligi hivyo tutapata muda wa kufanya marekebisho yaliyojitokeza mazoezini," amesema Mgunda.
Advertisement
Back to homepage
Share this story