Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya gym kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Januari Mosi.
Baada ya ushindi wa mabao 4-1 tuliopata dhidi ya KMC, Desemba 24 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora wachezaji walipewa mapumziko kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi kabla ya leo kurejea mazoezini.
Advertisement
Mazoezi ya gym husaidia kurejesha hali za utimamu wa mwili kwa wachezaji kabla ya kwenda uwanjani kujifunza mbinu mbalimbali.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo ikiwa ni hatua nzuri kwa benchi la ufundi kutoa mbinu kuelekea mechi dhidi ya Azam.