Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Januari (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Kiungo mkabaji Sadio Kanoute, kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho na mlinzi wa kati Henock Inonga ndiyo waliofanikiwa kuingia fainali ya kinyang'anyiro hicho.
Ndani ya mwezi Januari, Kanoute amecheza mechi saba sawa na Sakho huku Inonga akicheza nane huku wote wakionyesha kiwango bora.
Zoezi la mashabiki kupiga kura litaanza leo saa 12 jioni kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Jumatano Februari 2 saa 10 jioni.
Mshindi wa jumla atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa Wadhamini Emirate Aluminium ACP.
Kiungo Jonas Mkude ndiye aliyechukua tuzo hiyo mwezi Desemba huku Bernard Morrison akinyakua Novemba.