Baada ya uzinduzi wa jezi mpya za msimu ujao, uongozi wa klabu umeweka utaratibu mwepesi wa kusaidia wana Simba nchi nzima kuweza kununua jezi kupitia Simba App.
Kwa watakaonunua jezi kupitia Simba App kutakuwa na utaratibu maalumu wa kufikishiwa jezi popote pale nchini Tanzania. Watoa huduma wetu watawapigia simu wateja wote ndani ya masaa 24 ili kuwapa utaratibu wa kuweza kuwafikishia jezi.
Advertisement
Ili jezi iweze kumfikia mnunuzi wa ndani ya Dar es salaam kutakuwa na gharama ya ziada ya usafiri itakayolipiwa 5,000. Mashabiki wa nje ya Dar es salaam, watafikishiwa jezi hadi walipo kwa gharama ya usafiri ya 10,000.
Mbali na Simba App, jezi mpya pia zinapatikana kwenye maduka yote ya Vunja bei nchi nzima