Kocha Mkuu wa Timu ya Wanawake ya Simba Queens , Hababuu Ally ameweka wazi majina ya wachezaji 11 watakaoshuka dimbani kuikabili PVP FC Buyenzi ya Burundi katika mchezo wetu wa kwanza wa Caf Women's Champions League Cecafa Qualifiers 2021.
Mchezo huo utaanza saa 10 jioni katika Uwanja wa Nyayo ukitanguliwa na mechi ya kwanza ya kundi A kati ya Lady Doves dhidi ya FAD FC.
Kikosi cha Simba Queens kiliwasili hapa Kenya siku nne zilizopita hivyo wachezaji wameshazoea mazingira na wapo tayari kwa michuano hii mikubwa kwa wanawake barani Afrika.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
1. Janeth Shija
2. Doto Evarist
3. Fatuma Issa
4. Violeth Nicholas
5. Julieth Singano
6. Danai Bhobho
7. Asha Djafar
8. Joelle Bukuru
9. Mawete Musolo
10. Zena Khamis
11. Ruth Kipoyi
Wachezaji wa akiba
12. Zubeda Mgunda (Gk)
13. Maimuna Khamis
14. Violeth Thadeo
15. Jackline Albert
16. Shelda Boniface
17. Koku Kipanga
18. Silvia Thomas
19. Aisha Juma