Akizungumza kufuatia matokeo yetu ya sare dhidi ya Biashara United, Kocha Mkuu Didier Gomes, amewataka Wanasimba kuwa na umoja na kuacha kulaumiana.
Aidha, amekataa kumtupia lawama mtu yeyote katika sare tuliyopata jana dhidi ya Biashara United badala yake tuendeleze umoja ili kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa Ijumaa dhidi ya Dodoma Jiji.