Simba Sports Club
CAF Home Slide Latest News

DK. Gembe awatoa hofu Wanasimba kuhusu Manula

2 Mar 2021 By simbasc 974 views

Daktari wa timu, Yassin Gembe amewatoa hofu wapenzi na mashabiki kuhusu hali ya kiafya ya mlinda mlango namba moja Aishi Manula kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata majeraha jana.

Manula alitolewa dakika ya 65 baada ya kugongana na mshambuliaji wa JKT Tanzania, Danny Lyanga na kupelekea kupoteza fahamu na kukimbizwa Hospitali ambapo alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri.

Advertisement

Dk. Gembe amesema Manula anaendelea vizuri hakupata jeraha kubwa ingawa wanasubiri vipimo zaidi kujua hali yake na anataraji kuwepo kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Merreikh.

"Manula anaendelea vizuri jana aliumia kichwani lakini anaendelea vizuri tunasubiri vipimo zaidi na hakuna jambo la kuhofia zaidi," amesema Dk. Gembe.

Back to homepage
Share this story