Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye atakuwa mgeni rasmi katika mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa nne usiku.
Tumekuwa na utaratibu wa kualika viongozi mbalimbali wa Serikali katika mechi zetu za kimataifa lengo likiwa ni kuziongezea thamani.
Nape atawaongoza Wanasimba wote katika mchezo huo muhimu ambao tunahitaji ushindi pekee ili kutinga robo fainali.
Hata hivyo bado tunaendelea kusisitiza mashabiki kukata tiketi ili kujitokeza kwa wingi kuhamasisha wachezaji kuanzia mwanzo wa mchezo hadi mwisho.