Nane kuwakilisha nchi zao kufuzu AFCON

Wachezaji nane kutoka kwenye kikosi chetu wameitwa katika timu zao za taifa kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu michuano ya AFCON itakayofanyika mwakani.

Nyota watano mlinda mlango, Aishi Manula, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, Mzamiru Yassin na Kibu Denis wameitwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo itacheza mechi mbili dhidi ya Niger na Algeria.

Kiungo mshambuliaji Rally Bwalya ameitwa kwenye kikosi cha Timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambayo itacheza mechi mbili dhidi ya Ivory Coast na Comoro.

Mshambuliaji Medie Kagere amejumuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) ambayo itacheza dhidi ya Msumbiji na Senegal.

Winga Peter Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi (The Flames) ambayo itacheza na Ethiopia na Guinea.

Mechi hizo za kufuzu zitapigwa kati ya Juni 3 hadi Juni 14 kabla ya wachezaji kurejea kwa ajili ya kuendelea na mikiki mikiki ya Ligi Kuu ya NBC.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER