Mzizima Derby kupigwa Zanzibar Septemba 26

Mchezo wetu unaofuata wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC ‘Mzizima Derby’ utapigwa Septemba 26 katika Uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar saa 2:30 usiku.

Mchezo huo ulikuwa Haujapangiwa ratiba kutokana na ushiriki wa michuano ya Afrika kwa timu zote lakini sasa ni rasmi utapigwa Visiwani Zanzibar.

Maandalizi ya mchezo huo ambao ni muhimu kwetu yataanza mara tu tutakapomaliza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli utakaopigwa kesho.

Mchezo huo utakuwa ni wa tatu kwetu baada ya kushinda mechi mbili za kwanza dhidi ya Tabora United na Singida Fountain Gate.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER