Mzamiru: Wachezaji tuna ‘mzuka’ wa kutinga Nusu Fainali

Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin, ameweka wazi kuwa dhamira ya wachezaji wote ni kuhakikisha tunaitoa Orlando Pirates na kuingia Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mzamiru amesema tumewahi kufika robo fainali mara tatu lakini hatutafika nusu kwa hiyo safari hii ni malengo ni kuhakikisha tunavuka.

Mzamiru ameongeza kuwa wakiwa kambini hadi mazoezini mazungumzo yao ni kuhamasishana kuhakikisha wanapambana kuvuka hatua hii.

Kiungo huyo ameenda mbali zaidi na kusema asilimia kubwa ya wachezaji waliopo kikosini walikuwepo wakati tukifuzu robo fainali kwa hiyo malengo ya sasa ni kufika nusu fainali.

“Wengi wetu tulikuwepo mara tatu wakati tukiingia robo fainali lakini hatujawahi kufika nusu fainali, huu ndiyo wakati wetu kila mmoja yupo tayari. Sisi wenyewe morali yetu ipo juu na tupo tayari kutimiza malengo yetu,” amesema Mzamiru.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER