Mzamiru: Tuzo za Emirate zimeongeza kitu kikubwa kwa wachezaji

Mshindi wa mwezi Oktoba wa tuzo ya mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) Mzamiru Yassin amesema kila mchezaji anapambana kuipata na inaongeza morali.

Mzamiru ambaye ametwaa kwa mara ya kwanza amesema malengo yake yalikuwa ya kutwaa tuzo hiyo kwa kupambana kuisaidia timu na amefanikiwa.

Baada ya kufanikiwa kupata tuzo hiyo Mzamiru amesema haijaisha anataka kuchukua tena miezi inayokuja kwakuwa lengo kubwa ni kupambana kuisaidia timu.

“Tuzo za Emirate zimeongeza kitu kikubwa kwenye kikosi, kila mchezaji anapambana kuipata hivyo zinaongeza hamasa hadi uwanjani. Mimi nadhani ziendelee kuboreshwa lakini ni muhimu sana kwetu,” amesema Mzamiru.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano wa Emirate Aluminium Profile, Issa Maeda amempongeza Mzamiru kwa kushinda tuzo hiyo akiwa ni mzawa wa kwanza kuchukua kwa msimu huu.

“Kwanza Mzamiru ni mteja wetu mzuri, nyumba yake ameweka vifaa vya Emirate na tunawaomba wengine kufuata nyayo zake kwakuwa bidhaa zetu ni bora na bei yake ni nafuu,” amesema Maeda.

Katika mwezi Oktoba Mzamiru amecheza mechi tano sawa dakika 450 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa moja jingine.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER