Mzamiru Mchezaji Bora wa Emirate Oktoba

Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki mwezi Oktoba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Mzamiru amewashinda kiungo mshambuliaji, Augustine Okrah na mlinzi wa kati Joash Onyango ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Oktoba Mzamiru amecheza mechi tano sawa dakika 450 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa moja jingine.

Mchanguo wa kura ulivyokuwa

Kura Asilimia

Mzamiru 4274 64.60

Okrah 1361 20.57

Joash 981 14.83

Kwa kuibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro hicho Mzamiru atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 pamoja na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER