Mzamiru, Kapombe, Kanoute wachuana Mchezaji Bora Novemba

Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha kutafuta mchezaji bora wa mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) wa mwezi Novemba.

Wachezaji hao ni viungo wakabaji Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute pamoja na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

Walinzi wawili Joash Onyango na Mohamed Hussein wameingia tano bora lakini baada ya mchujo ndiyo wamebaki watatu waliongia fainali.

Takwimu za wachezaji wote za mwezi Novemba

Mechi   Dakika  Mabao  Assist

Mzamiru     6            530         1            1

Kapombe    6           540         1            0

Kanoute       5           398         0            0

Zoezi la kupiga kura kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz litaanza leo Novemba 28 saa 7 mchana na litafungwa Desemba Mosi mwaka huu.

Mshindi ni yule atakayepata kura nyingi ambapo atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER