Mzamiru atoa neno kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC

Kiungo Mzamiru Yassin amekiri kuwa mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu lakini tutashinda na kutinga fainali.

Mzamiru amesema mara zote mechi za nusu fainali huwa ngumu kutokana na kila timu kuamini inaweza kuingia fainali lakini ubora wa kikosi chetu unampa matumaini ya kuibuka na ushindi.

Kiungo huyo ameongeza kuwa tutaingia uwanjani kwa kuiheshimu Azam sababu ni timu bora na tunafahamu watatupa upinzani mkubwa lakini hata hivyo tumejipanga kuwakabili.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Azam ni timu nzuri na inatupa ushindani mkubwa lakini tumejipanga kuwakabili na lengo letu ni moja kuingia fainali na tutapambana kuhakikisha tunafanikisha,” amesema Mzamiru.

Mchezo huo utafanyika katika Uwanja wa Majimaji hapa Songea, Jumamosi Juni 26, saa tisa alasiri.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER