Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia katika kikosi chetu.
Mkataba wa Mzamiru umemalizika mwishoni mwa msimu huu na mapendekezo ya kiufundi yamependekeza mchezaji huyo kubaki kutokana na mchango wake, hivyo uongozi umemuongezea miaka mingine miwili ya kuendelea kusalia kikosi
Mzamiru ni sehemu ya mpango wa timu wa kusuka kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao
Mzamiru ni katika wachezaji waandamizi waliodumu ndani ya Simba kwa muda mrefu zaidi akihudumu kwa miaka nane kwa kiwango bora na sifa yake kubwa ikiwa kujituma na usikivu.