Mzamiru afunguka mipango ya Afrika

Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin, amesema kwa sasa malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Premeiro De Agosto Jumapili ili kufuzu hatua ya makundi.

Mzamiru amesema msimu uliopita tulishindwa kufika hatua ya makundi tukaangukia Kombe la Shirikisho ndiyo maana msimu huu hamasa ni kubwa kuanzia kwa uongozi, wachezaji mpaka mashabik ili kufanikisha.

Mzamiru ameongeza kuwa pamoja na kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza Angola lakini mechi ya Jumapili itakuwa ngumu kwa kuwa De Agosto watakuwa hawana cha kupoteza zaidi ya kutafuta ushindi.

“Malengo yetu kama klabu kwanza ni kufuzu hatua ya makundi, ni kweli tumepata ushindi mzuri ugenini na tunajua mchezo wa Jumapili utakuwa mgumu lakini tumejipanga.

“Tumepata maandalizi mazuri na sisi wachezaji tupo tayari kuhakikisha tunafanya tunaloweza kuwapa furaha Wanasimba Jumapili,” amesema Mzamiru.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER