Mzamiru afunguka kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Jumamosi

Kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin amesema ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Manungu Complex.

Mzamiru amesema maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri na wachezaji wapo kwenye hali nzuri kupambana kupata alama tatu.

Mzamiru amesema anajua mchezo utakuwa mgumu kutokana n ubora wa Mtibwa hasa wakiwa katika uwanja wa nyumbani lakini tupo tayari kwa mpambano.

“Ligi inaelekea ukingoni na kila timu imejipanga kutafuta pointi tatu, tunafahamu tunakutana na Mtibwa ambayo inahitaji alama tatu lakini tumejiandaa kikamilifu kuwakabili.

“Kwa sasa tunahitaji ushindi katika kila mchezo uliobaki, hatuhitaji kupoteza alama yoyote kwakuwa bado malengo yetu ni kuchukua ubingwa,” amesema Mzamiru.

Tayari kikosi cha wachezaji 25 kimewasili salama mkoani Morogoro tayari kwa mchezo huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER