Mwitikio wa Wanasimba waushangaza uongozi

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema uongozi umeshtushwa na jinsi Wanasimba walivyohamasika katika kuchangia ujenzi wa uwanja.

Amesema Wanasimba wakiamua jambo lao hawarudi nyuma hatua ambayo itakamilisha lengo la kumiliki uwanja wetu haraka zaidi ya ilivyodhaniwa.

Mwenyekiti amesema uongozi utaunda Kamati maalumu kwa ajili suala hilo ambapo itakuwa na kazi ya kuandaa bajeti na michoro ili ujenzi uanze mara moja.

“Kwa niaba ya uongozi tunawashukuru Wanasimba wote waliochangia kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wetu, mwitikio ni mkubwa na hamasa ni kubwa, hii ndiyo maana ya Nguvu moja.

“Uongozi tumeshtushwa na hatua hiyo kubwa hatukutegemea. Tunategemea kukamilisha jambo hili haraka zaidi ya tulivyotarajia.

“Pamoja na mambo mengine, tunaandaa utaratibu kwa ajili ya Wanasimba walio nje ya Tanzania kuchangia,” amesema Try Again.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. Ningeshauri hili jambo la kuchangia uwanja mpeleke matangazo kwenye vituo vya radio ili kuongeza hamasa zaid.
    Simba nguvu moja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER