Mwana FA akabidhi pesa za goli la mama

Naibu Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Mh. Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amemkabidhi nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ milioni 10 kwa ajili pesa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ‘Bao la Mama’.

Rais Samia hutoa Shilingi milioni tano kwa kila bao litakalofungwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kuongeza morali kwa wachezaji.

Bao la mama limeongeza morali kwa wachezaji kujituma kuisaidia timu kupata matokeo ya ushindi.

Katika mchezo wa leo dhidi ya Wydad Casablanca mabao yote mawili tuliyoshinda yamefungwa na kiungo mshambuliaji, Willy Onana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER