Mshambuliaji Asha Rashid ‘Mwalala’ amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi mnono wa 5-0 tuliopata dhidi ya FAD Djibouti katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki uliopigwa katika Uwanja wa Abebe Bikila.
Jentrix Shikangwa alitupatia bao la kwanza dakika ya 24 baada ya kuunganisha Kwa mguu wake wa Kushoto krosi iliyopigwa na Fatuma Issa.
Elizabeth Wambui alitupatia bao la pili dakika ya 30 baada ya kupiga shuti kali lilomshinda Kipa wa Fad kufuatia kupokea Pasi Ya Precious Christopher.
Asha Rashid ‘Mwalala’ alitupatia bao la tatu dakika ya 73 kutoka upande wa kulia Kwa Shuti kali lilomshinda Golikipa Soubane Ahmed.
Dakika 80 ya Mwalala alifunga bao nne baada ya Kupokea pasi ya Jackline Albert akiwa ndani ya 18.
Mwalala ailikamilisha hat trick yake baada ya kufunga bao la tano dakika ya 90 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa FAD.
Kocha Mkuu Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Jackline Albert, Mwanahamisi Omary, Mwalala, Shelda Boniface na Esther Mayala na kuwatoa Precious Christopher, Amina Bilal, Ritticia Nabbosa, Jentrix Shikangwa na Violeth Nicholas.