Mshambuliaji Steven Mukwala amesema licha ya hali ya hewa kuwa baridi kali nchini Algeria lakini tutaizoea hadi kufika Jumapili siku ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine.
Mukwala amesema hali ya hewa ni tofauti na jijini Dar es Salaam lakini anaamini mpaka kufika Jumapili watakuwa wamezoea na haitakuwa changamoto tena.
Akizungumzia kuhusu hali ya wachezaji baada ya safari ndefu amesema wako tayari kukamilisha programu ya mazoezi hapa Algeria kabla ya kushuka dimbani siku ya Jumapili.
“Tumefika salama Algeria, kikubwa mashabiki wa Simba watuombee tuweze kuwa salama muda wote ili kuipambania timu yetu na kuwapa furaha Wanasimba wote,” amesema Mukwala.