Mugalu, Morrison kuongoza mashabulizi dhidi ya USGN

Mshambuliaji Chris Mugalu na kiungo mshambuliaji Bernard Morrison wataongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo wetu wa leo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi y US Gandarmerie kutoka Niger utakaoanza saa nne usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo wengine wawili washambuliaji Pape Sakho na Rally Bwalya.

Kocha Mkuu Pablo Franco ameanzisha idadi kubwa ya viungo washambuliaji lengo likiwa ni kutengeneza nafasi nyingi ambazo zitazalisha mabao.

Katika eneo la kiungo wa ulinzi Pablo amewaanzisha Jonas Mkude na Sadio Kanoute kama ilivyo kawaida katika mechi zetu za karibuni.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (17), Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7), Rally Bwalya (8), Bernard Morrison (3)

Wachezaji wa akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Taddeo Lwanga (4), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Peter Banda (11).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER