Mshambuliaji Chris Mugalu amepewa dhamana ya kuongoza mashambulizi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa leo saa 10 jioni katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Mugalu hajaonekana uwanjani katika mechi mbili za ligi zilizopita lakini leo kocha Didier Gomez amempa dhamana ya kuhakikisha anaongoza idara ya ushambuliaji.
Kiungo mkabaji Taddeo Lwanga nae amerejea kikosini baada ya kukosekana katika mechi iliyopita huku Hassan Dilunga pia akianza.
Luis Miquissone ambaye ni mchezaji bora wa ligi wa mwezi Machi, alipumzishwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC naye ameanza pamoja na pacha wake Clatous Chama wakiwa na kazi ya kumlisha Mugalu.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohammed Hussein ©
4. Joash Onyango
5. Pascal Wawa
6. Taddeo Lwanga
7. Hassan Dilunga
8. Mzamiru Yassin
9.Chris Mugalu
10. Clatous Chama
11. Luis Miquissone
Wachezaji wa Akiba
GK. Beno Kakolanya
02. Erasto Nyoni
03. Ibrahim Ame
04. Rally Bwalya
05. Medie Kagere
06. John Bocco
07. Ibrahim Ajib
2 Responses
All the best wanajeshi wetu
Congratulations to Simba Team. We need Success to all our games. And we pray to OUR GOD for this success. Aamin