Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Yanga Leo

Mshambuliaji Chris MugaluĀ  ataongoza mashambulizi katika mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza saa tisa alasiri.

 

Mugalu atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji wawili Kibu Denis na Pape Sakho ambao watatokea pembeni.

 

Katika eneo la kiungo wa kati kocha Pablo Franco amewapanga viungo watatu Taddeo Lwanga, Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

 

Mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya atasimama katika milingoti mitatu akichukua nafasi ya Aishi Manula ambaye ameumia vidole viwili vya mkono.

 

Kikosi Kamili kilivyopangwa

 

Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Taddeo Lwanga (4), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38).

 

Wachezaji wa Akiba

 

Ally Salim (1), Aishi Manula (28), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER