MUGALU KUONGOZA MASHAMBULIZI DHIDI YA JKT LEO

Mshambuliaji Chris Mugalu ataongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mugalu ambaye kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza alikuwa kwenye orodha ya wafungaji katika ushindi wa mabao 4-0 kule Jamhuri, Dodoma hakuonekana uwanjani tangu mechi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Kiungo Taddeo Lwanga nae ameanza kwenye kikosi cha kwanza tangu mchezo dhidi ya Al Ahly ukiwa ni utaratibu wa kocha Didier Gomez kumpa kila mchezaji muda wa kucheza.

Kikosi Kakimili kilivyopangwa

 1. Aishi Manula
 2. Shomari Kapombe
 3. Mohamed Hussein
 4. Erasto Nyoni
 5. Pascal Wawa
 6. Kennedy Juma
 7. Clatous Chama
 8. Taddeo Lwanga
 9. Chris Mugalu
 10. Mzamiru Yassin
 11. Luis Miquissone

Wachezaji wa Akiba

GK.  Beno Kakolanya

02. David Kameta

03. Ibrahim Ajib

04. Medie Kagere

05. Perfect Chikwende

06. Rally Bwalya

07. John Bocco

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER