Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi KMC leo

Mshambuliaji Chris Mugalu amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wa leo wa ligi kuu dhidi ya KMC utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Katika mchezo uliopita Mugalu alitokea benchi kutokana na majeruhi lakini leo Kocha Didier Gomes amempa nafasi ya kuanza.

Viungo washambuliaji Clatous Chama, Luis Miqiussone na Rally Bwalya watakuwa na wajibu wa kumrahisishia kazi Mugalu.

Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin wao wamepangwa katika eneo la kiungo wa ulinzi kuhakikisha mabeki wetu hawafikiwi kirahisi.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Chris Mugalu (7), Rally Bwalya (8), Luis Miqiussone (11).

Wachezaji wa Akiba: Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Hassan Dilunga (24), Medie Kagere (14), John Bocco (22), Bernard Morrison (3)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER