Mugalu arejea Simba ikijiwinda na mtani

Mshambuliaji wetu Chris Mugalu amefanya mazoezi pamoja na wenzake leo jioni baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.

Mugalu alikosa baadhi ya mechi zilizopita za hivi karibuni zilizopita kutokana na majeraha hayo.

Mbali na Mugalu, wachezaji wengine wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu isipokuwa tutaendelea kukosa huduma ya Ibrahim Ajibu ambaye ni majeruhi na Jonas Mkude suala lake la kinidhamu bado halijamalizika.

Kikosi chetu kinajiandaa na mchezo na watani wa jadi Yanga ambao utafanyika Jumamosi Julai 3, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.

Tayari kikosi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo muhimu ambao kama tukishinda tutatawazwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mara ya nne mfululizo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Nguvu Moja Na Mungu Atupe Uzima Tuwe Wenye Afya Njema Na Tuweze Kushiriki.Vyema Kwenye Derby Na Mungu Atujaaliye Ushindi Mnono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER