Mugalu arejea, kuongoza mashambulizi dhidi ya Dodoma leo

Baada ya kutopata nafasi kwenye mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Biashara United mshambuliaji Chris Mugalu ataongoza mashambulizi kwenye mechi ya leo dhidi ya Dodoma Jiji itakayopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri saa 10 jioni.

Mugalu alikuwa benchi kwenye mchezo huo huku Kocha Didier Gomes akiwaanzisha Medie Kagere na John Bocco.

Kocha Gomes amekuwa akiamini kwenye matumizi ya mshambuliaji mmoja akisaidiwa na viungo watatu wa ushambuliaji huku Mugalu akimpa nafasi zaidi.

Kiungo Taddeo Lwanga naye amerejea kikosini baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu ambapo leo ameanza akisaidiana na Mzamiru Yassin.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5)
Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Yusuph Mhilu (27), Mzamiru Yassin (19), Chris Mugalu (7), Pape Sakho (17), Hassan Dilunga (24)

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Henock Inonga (29), Rally Bwalya (8), Duncan Nyoni (23), Medie Kagere (14), John Bocco (22), Jimmyson Mwinuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER