Mugalu ang’ara tuzo za VPL Julai

Mshambuliaji Chris Mugalu amechaguliwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wa mwezi Julai.

Mugalu amekuwa kwenye kiwango bora ndani ya mwezi Julai ambapo amefunga mabao matano katika mechi tano tulizocheza.

Mugalu raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amewashinda Charles Ilamfia wa KMC na Juma Luizio wa Mbeya City ambao aliingia nao fainali.

Hii ni tuzo ya kwanza ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu kwa Mugalu tangu ajiunge nasi mwanzoni mwa msimu huu.

Wachezaji wetu wengine waliowahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi ni pamoja na Nahodha John Bocco aliyeshinda mara mbili, Clatous Chama na Luis Miquissone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER