Motsepe: AFL imekuja kuongeza uchumi wa klabu

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Patrick Motsepe amesema lengo la michuano ya African Football League (AFL) ni kuzisaidia klabu za Afrika kiuchumi.

Motsepe amesema timu zinazoshiriki michuano hiyo zinapatiwa kiasi kikubwa cha pesa na zile zinazofanya vizuri zaidi inakuwa kubwa zinaweza kuisaidia kufanya vitu vikubwa zaidi.

Motsepe ameongeza kuwa AFL haitaiua michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kama wengi wanavyodhani badala yake imeanzisha ili kuziongezea klabu uwezo wa kiuchumi.

“Moja ya malengo ya AFL ni kuzisaidia klabu kiuchumi sababu tunalipa kiasi kikubwa, mipango yetu ni kuzifanya klabu za Afrika zijiendeshe kisasa.”

“Idadi kubwa ya wachezaji kutoka Afrika wanatamani kucheza soka barani Ulaya sababu ya malipo mazuri nasi tunataka Afrika tufike kwenye hatua hiyo,” amesema Motsepe.

Motsepe amethibitisha mwakani michuano ya African Football itashirikisha timu 24 badala ya nane ambazo zitashiriki msimu huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER