Moto wa Simba Queens usipime

Timu yetu ya Wanawake Simba Queens imeendelea kutoa dozi katika Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) baada ya kuichakaza bila huruma TSC Queens mabao 4-0 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukitengeneza nafasi za kufunga ingawa idara ya ushambuliaji haikuweza kuzitumia zote.

Mshambuliaji mpya Olaiya Barakat Kutoka Nigeria alitupatia bao la kwanza dakika ya 15 baada ya juhudi binafsi kuwapiga chenga mabeki kabla ya kufunga.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuongeza mabao matatu yaliyofungwa na Asha Djafar, Joelle Bukuru na Danai Bhobho.

Kocha Sebastian Nkoma alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Jackline Albert, Olaiya Barakat na Pambani Kuzoya na kuwaingiza Amina Ramadhani, Asha Djaffar na Opah Clement.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha pointi 18 baada ya kushinda mechi zote sita tulizocheza na kuendelea kusalia kikeleni.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER