Morrison, Mkude, Kagere wachuana Mchezaji Bora Novemba

Nyota wetu watatu Bernard Morrison, Jonas Mkude na Medie Kagere wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Kuchaguliwa kwa wachezaji hao kumetokana na uwezo mkubwa walioonyesha katika mechi tulizocheza Novemba.

Awali walikuwa wachezaji watano akiwamo walinzi Joash Onyango na Mohamed Hussein lakini wamechujwa na Kamati Maalumu na kubaki watatu ambao watakaopigiwa kura na mashabiki kupitia tovuti rasmi ya klabu ya www.simbasc.co.tz

Zoezi la kupiga kura limefunguliwa leo na litafungwa Desemba Mosi saa 10 jioni ambapo atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.

Hassan Dilunga aliibuka mshindi wa mwezi Oktoba na kujinyakulia kitita cha Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini wa tuzo Emirate Aluminium ACP.

This poll has ended (since 2 years).
SHARE :
Facebook
Twitter

15 Responses

  1. Naupongeza management nzima ya Simba kwa kazi nzuri kutuletea kocha bora Mr. Pablo.

    Maoni yangu kwa Management ya Simba wafanye haraka iwezanavyo kocha bora wa makipa haraka ili kulinda uwezo wa makipa wetu usishuke.
    By Marwa from Dubai

  2. Kwa kweli kocha tunaye, nadhani malengo yetu ya kufika semi finals caf confederation cup inawezekana wachezaji wakijituma kama jana. Pongezi kwa management na timu kwa ujumla mnatupa raha

  3. Naomba kupewa nafasi linapoandaliwa dua la kuimbea simba,
    Kuwe na maombi ya wakristo mashabiki na viongozi wa simba, na Waimbaji ILI KUONGEZA UFATILIWAJI, HAMASA, NA UMWAMBA WA TIMU NDANI NA NJE.

  4. Tunawataki mchezo mwema kesho wachezaji wetu. Sisi tuko nyuma yenu tunaomba mjitume kwani pointi tatu ni muhimu sana kwetu kwa Sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER