Morrison, Miquissone, Bocco mchuano mkali Tuzo ya Mchezaji Bora

Nyota watatu Bernard Morrison, Luis Miquissone na John Bocco wameingia fainali ya kumsaka Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Juni (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Kabla ya mchujo wa Kamati Maalumu ya tuzo hizo,  nyota hao walikuwa watano akiwamo Rally Bwalya na Pascal Wawa.

Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa mshabiki inadhaminiwa na Kampuni ya Emirate Aluminum Profile ambayo ilianza kutolewa Februari mwaka huu.

Mshindi kati ya nyota hao watatu ni yule atakayepata kura nyingi zitakazopigwa na mashabiki kupitia tovuti hii rasmi ya klabu.

Zoezi la kupiga kura litaanza leo usiku na litakamilika Julai 1 Mosi usiku na mshindi atakayetangazwa atajinyakulia kitita cha Sh 1,000,000 kutoka Emirate Aluminum Profile.

This poll has ended (since 3 years).

Emirate Aluminium Simba Fans Player of The Month

Bernard Morrison
69.13%
Luis Miquissone
23.41%
John Bocco
7.46%
SHARE :
Facebook
Twitter

55 Responses

 1. Please at all cost keep Lui Miqquison for this coming season, we need strong squad for the cuf champion league.

 2. Fungueni Matawi ya Simba sc kila Kata Kijiji,Mtaa by
  Mwakinyuke nipo MBARALI kata ya MAPOGORO
  Kijiji Cha UKWAVILA
  Kitongoji Cha IBOHORA
  MOBILE NUMBER +255789171900
  +255763803300

 3. Kwa mwezi huu morrison anastahili sana. Mechi ya nusu fainal dhidi ya Azam iliamriwa na uzoefu wake. Hata miquissone alipata confidence ya kugunga lile goli kisa BM3

 4. Hongera sana Prof.Gomes kwa kazi nzuri unayoifanya,,,ila nakushauri uwe makini katika kuchagua wachezaji wa kuacha na kusajili tunapoelekea mwisho wa msimu ili kulinda hadhi ya klabu ya Simba ambayo kiukweli IPO juu kwa sasa./Congratulations Prof. Gomes for the good job that you are doing in simba sports club,I advice you to be careful in sorting players to sign and those ones to extend their contracts as we are going to the end of 2020 /2021 season! So as to continue keeping Simba’s status!

 5. Tunaomba mwongozo kwa mashabiki wenu wa mikoani namna ya kupata kadi za uanachama na jinsi ya kulipia ikiwezekana hata kutengeza mfumo wa kizipata online. Kutoka Chimala Mbarali Mbeya

 6. SIMBA SC fungueni matawi kuanzia kitongojini,vijijini,katani mpate wanachama wengi Sana kila mkoa
  Mimi Ni Mwakinyuke .
  Nipo Mbarali
  Kata ya Mapogoro
  Kijiji ch Ukwavila
  kitongoji Cha Ibohora
  Namba ya Simu Ni
  +255789171900
  +255763803300

 7. Viongozi walioko mitaani , katani, wilayani na mikoani iwepo sababu.ya kuwa na ofisi katika sehemu hizo. Ili kujua idadi halisi ya mashabiki. Simba ni timu kubwa!

 8. Mchezaji ambaye hana skendo toka amejiunga na Simba kwa kwel me mzalendo aise Bocco binafsi namuelewa sana

 9. SANYIWA MWINAMILA NZUGAMAWE 0745769430 NIPO MPANDA KATAVI VIJIJINI TUNATA TAWI NAKADI ZACHAMA SIMBA NGUVU MOJA🙏

  1. Kutoka Znbr Binafsi Simba naipenda sana na Siku tukipoteza mchezo naumwa na kichwa sana nakuwa nashindwa kufanya chochote kwa siku hiyoo

  2. Kutoka Znbr Binafsi Simba naipenda sana na Siku tukipoteza mchezo naumwa na kichwa sana nakuwa nashindwa kufanya chochote kwa siku hiyoo

 10. Nashauri kwenye hili suala la mchezaji bora wa mwezi wa mashabiki,baada ya ule mchujo wa kwanza kufanyika wakibaki watatu wanao shindanishwa,Naomba muwe mnaweka na takwimu zao pia na itapendeza pia ikiwa kwa idadi sawa ya mechi hii itasaidia kupata mshindi sahihi

 11. Simba mnafeli sehemu mojaa asee club yangu, lipeni hamasa swala la kuwa na kadi za uanachama active… Tuzunguke taifa zima tuwape wanachama kadi ili tuingize mapato ya kutoshaaa…. Binafsi natamani kuona simba ikiwa na uwanja mzuri, nyumba nzuri za wachezaji na mishahara minonoo… Wakati ndio huu ambao mashabiki wako na amasa na timu na inafanya vizuri tuzunguke tukusanye pesa kutoka kwenye kadi za uanachama taifa zima tutapata billions ambazo zitatusaidia sana kwenye mambo makubwa ukiachana na mdhamini, get collection na hela za champions league
  Nina imani ujumbe wangu utafanyiwa kazi 🙏
  #nguvumoja

 12. Brothers and Sisters klabu ya Simba ndiyo tulizo la mioyo yetu! Hatujafanya makosa kwenye kuishabikia klabu hii, lakini itakuwa ni ajabu kama tutashindwa kujivunia klabu yetu na kuiunga mkono… vile vile viongozi waweke wazi klabu yetu inaingiza kiasi gani na matumizi yapoje kwa maana ipo siku tutajikuta tuko chali…. 🦁🔥

 13. Utaratibu wa tuzo za mchezaji Kwa mashabiki unavutia na kupendeza pia unaleta chachu Kwa wachezaji

 14. Katika kurasa rasmi ya Simba SC ningependa kuulizia kuhusu mwenendo wa mabadiliko ndani ya klab yetu umefikia wapi na kama kuna changamoto sisi mashabiki,wanachama na wapenzi wa Simba kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi tutafute suluhu kwa pamoja, itakua aibu kama mchakato wa Yanga utaenda smooth na kutupita sisi tulioanza.
  Ahsante

 15. Ninaoongeza utaratibu wa utoaji tuzo, uko huru na uwazi. Utaongeza bidii kwa wachezaji wetu.

  Nitumie nafasi hii adhimu pia kuongeza namna uongozi wa SIMBA SC unavyoendesha mambo kiuweledi na kudhihirisha timu imekuwa kubwa kiasi gani.

  Viva Simba SC, #Nguvu Moja#

 16. Kutoka Znbr Binafsi Simba naipenda sana na Siku tukipoteza mchezo naumwa na kichwa sana nakuwa nashindwa kufanya chochote kwa siku hiyoo

 17. A very good platform for players to get motivated more and obviously it increase team performance that led to good results of the team! Congratulations to those who brought this!#Nguvu Moja

 18. Napendekeza sisi Kam klabu ya Simba tuwe na Simba Archives (Jengo) ionyeshwe kweny televishen yetu ya Simba TV, itakayotunza na kuonyesh historia mbalimbali za klabu yetu.

 19. Utaratibu huu ni mzuri sana ingawa changamoto ni pale inapotokea waliowekwa au wanaowekwa wote wanamchango mkubwa kwa kila mechi but kwa inshu ya juzi na Azam acha nimpe Morrison.

 20. Morrison anadiserve kuwa Bora mwezi huu hata uliopita cos kaonyesha kile alichonacho pia anacheza kwa moyo

 21. Ningeomba kama itawezekana mje kutufungulia Tawi la Simba njiro Arusha maana mashabiki tunaoipenda Simba tupo wengi mno huku

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER