Morrison akabidhiwa tuzo yake na Emirate Aluminum ACP

Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison, amekabidhiwa tuzo yake mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Novemba na wadhamini Emirate Aluminum ACP.

Morrison amekabidhiwa kitita cha Sh 2,000,000 kama sehemu ya zawadi kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Morrison ameshinda tuzo hiyo kutokana na kuwa na kiwango bora katika mwezi huo akichangia kupatikana kwa mabao manne akifunga mawili na kusaidie mengine mawili.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Morrison amewasifu wachezaji alioingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho kuwa kila mtu alistahili kushinda lakini mshindi siku zote ni mmoja hivyo amefurahi kushinda.

“Nawapongeza pia nilioingia nao fainali wote tulistahili kushinda lakini mimi nimeibuka kidedea, nimefurahi na hii inanifanya kuendelea kujituma kuisaidia timu,” amesema Morrison.

Ofisa Uhusiano wa Emirate Aluminium ACP, Issa Maeda amesema mwezi Novemba kulikuwa na mchuano mkubwa wa kura kati ya Morrison na Medie Kagere na hivyo ndivyo bidhaa zao zinavyofanya vizuri sokoni.

“Ukiangalia mchuano wa kura utagundua tuzo hizi zinafuatiliwa na watu wengi hata bidhaa zetu zinafuatiliwa kwa wingi sokoni hilo ndilo jambo linalo tuvutia zaidi,” amesema Maeda.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. It’s amazing to pay a visit this web site and reading the
    views of all colleagues about this paragraph, while I am also keen of getting know-how.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER