Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ameanzishwa katika kikosi cha kwanza kilichopangwa kuikabili Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa leo saa 11 jioni.
Morrison ‘Mzee wa kukera’ mara kadhaa amekuwa akianzia upbenchi na kuingia kipindi cha pili kubadili mchezo lakini leo kocha Didier Gomes ameamua kumuanzisha.
Mbali na uwezo mkubwa alio nao Morrison lakini katika kipindi hiki yupo kwenye kiwango bora ndiyo maana benchi la ufundi limeamua kumuanzisha dhidi ya Yanga.
Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza mashambulizi akisaidiana kwa karibu na viungo Clatous Chama, Luis Miquissone pamoja na Morrison.
Katika idara ya kiungo wa ulinzi Taddeo Lwanga ameendelea kuaminiwa na leo atacheza pamoja na mkongwe Erasto Nyoni.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Bernard Morrison (3), Erasto Nyoni (18), John Bocco (22), Clatous Chama (17), Luis Miquissone (11).
Wachezaji wa Akiba: Beno Kakolanya (30), Kennedy Juma (26), Mzamiru Yassin (19), Hassan Dilunga (24), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Chris Mugalu (7).
2 Responses
God bless us we are simba
Umaliziaji Simba haukuwa wa kiwango. Magoli mengi yalikoswa kipindi chapili