Mo: Tunashinda pamoja, Tunafungwa pamoja

Rais wa Heshima na muwekazaji wa klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema hatupaswi kukata tamaa baada ya jana kupoteza nyumbani dhidi ya Raja Casablanca.

Mo amesema tunatakiwa kuendelea kuwaunga mkono wachezaji wetu na kuwapa sapoti sio kuwavunja mkono.

Mo ameongeza kuwa sio mara zote utapata matokeo mazuri kwahiyo tunapaswa kukubaliana na kila hali.

“Simba tunafunga pamoja, tunafungwa pamoja. Hatukati tamaa. Tutaendeleza mapambano,” amesema Mo.

Kikosi kitashuka dimbani Jumanne kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi ya NBC utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER