Mo: Hakuna kurudi nyuma, mapambano yanaendelea

Rais wa Heshima wa Klabu na muwekezaji, Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema licha yakuwa hatukuwa na msimu mzuri lakini hatupaswi kurudi nyuma badala yake kuboresha kwenye mapungufu yaliyojitokeza.

Mo amesema kwa miaka mitano iliyopita tumekuwa na mafanikio makubwa na bajeti iliongezeka mara tano ambapo tumeshinda mataji ya ndani huku tukiweka alama Kimataifa kwa kufika Robo Fainali tatu za michuano ya Afrika.

Mo ameongeza kuwa baada ya mafanikio hayo lazima kikosi kifanyiwe marekebisho kadhaa kutokana na wachezaji kutumika muda mrefu ili kurudi katika mstari wa kuendelea kuipambania mataji.

“Hakuna kurudi nyuma, tunatakiwa kufanya mabadiliko katika maeneo ambayo tuna mapungufu na kwenda mbele. Mapambano yanaendelea wala hakuna kukata tamaa,”

“Najivunia kuweza kusema tupo katika orodha ya klabu bora 12 barani Afrika . Hii imekuwa mara ya kwanza Simba kuwa na mwendelezo mzuri katika miaka 86 ya historia yetu hatupaswi kubweteka badala yake kupambana kufikia malengo tuliyojiwekea,” amesema Mo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER