Mo awatembelea wachezaji kambini

Rais wa Heshima na muwekazaji wa klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amewatembelea wachezaji kambini kwa ajili ya kuwapa hamasa kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Mo amewakumbusha wachezaji kuhakikisha wanapambana hadi mwisho ili tupate ushindi katika mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu.

Mo amewaambia wachezaji Wanasimba wote ndani na nje ya nchi wanategemea kupata furaha kesho na wao ndio wanaweza kulikamilisha jambo hilo.

“Kesho mkiingia uwanjani mnatakiwa mjue furaha ya Wanasimba ipo mabegani kwenu, mnapaswa kujitoa ili jambo hili likamilike.

“Wote tunajua mchezo utakuwa mgumu, Raja ni timu nzuri lakini mnatakiwa kupambana na mimi nawaamini na Wanasimba pia wanawaamini kwahiyo msituangushe,” amesema Mo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER